Jinsi ya Kujisajili Ajira Portal

Mwongozo wa Kufungua Account Ajiraportal. Ajira Portal ni jukwaa la mtandaoni lililoundwa na sekretarieti ya ajira Tanzania ili kuwawezesha wanaotafuta kazi kutuma maombi ya nafasi wazi katika taasisi na mashirika mbalimbali ya serikali.

Hatua za Kujisajili (Create Account)

  1. Tembelea tovuti rasmi: https://portal.ajira.go.tz.
  2. Bonyeza “Register”: Chagua kitufe cha Register ili kufungua fomu ya usajili.
  3. Jaza fomu: Ingiza barua pepe halali na nenosiri ambalo utalitumia kuingia.
  4. Thibitisha nenosiri: Rudia nenosiri kwa uhakika.
  5. Thibitisha barua pepe: Fungua barua pepe uliyopokea na bonyeza kiungo cha uthibitisho.
  6. Hifadhi taarifa zako: Weka barua pepe na nenosiri mahali salama.
Links Mhimu
  1. Matangazo ya Kazi
    Link: https://portal.ajira.go.tz/vacancies
    Hii ni sehemu yenye matangazo ya kazi, ambapo waombaji wanaweza kuona kazi zote zilizotangazwa kwenye Ajira Portal.
  2. Kuingia kwenye Akaunti
    Link: https://portal.ajira.go.tz/auth/login
    Hii ni link ya kuingia kwa watumiaji waliosajiliwa tayari.
  3. Maoni na Mrejesho
    Link: https://portal.ajira.go.tz/feedback
    Hii ni sehemu ya kutoa maoni na mrejesho kuhusu uzoefu na huduma zinazotolewa kwenye Ajira Portal.
  4. Kujisajili kwa Akaunti Mpya
    Link: https://portal.ajira.go.tz/auth/register
    Hii ni kwa waombaji wapya wanaotaka kujiandikisha kwenye Ajira Portal.