UCHAMBUZI WA RIWAYA YA VUTA N'KUVUTE

vutanikuvute-810x907.png


UHAKIKI WA RIWAYA YA "VUTA N'KUVUTE”

WACHAPISHAJI: MKUKI NA NYOTA


MWANDISHI: ADAM SHAFI ADAM

MWAKA: 1999


UTANGULIZI


Vuta n'Kuvute ni riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na mwandishi mahiri na mkongwe Shafi Adam Shafi na kuchapishwa kwa mara ya kwanza na Mkuki na Nyota Publishers Dar es Salaam.

Adam Shafi ni mwandishi wa Fasihi ya Kiswahili ambaye ameandika kazi nyingi na miongoni mwa kazi zake nzuri alizowahi kuandika ni Kuli na Kasri ya Mwinyi Fuad. Riwaya ya Vuta n'Kuvute imejikita juu ya Vuta ni Kuvute za kisiasa, kiutamaduni na kijamii.vuta n'kuvute hizi zimeweza kuibua dhamira mbalimbali ambazo mwandishi alikusudia ziifikie jamii aliyoiandikia. Pia mwandishi ametumia ufundi mkubwa wa kisanaa katika kuzielezea dhamira.

Maudhui​

Dhamira kuu: Ukombozi

Katika riwaya hii, mtunzi anajadili aina nne za ukombozi ambazo ni ukombozi wa kiutamaduni, ukombozi wa kisiasa, ukombozi wa kiuchumi na ukombozi wa kifikra.

Ukombozi wa kiutamaduni​

Katika kujadili ukombozi wa kiutamaduni, mwandishi anaonesha kuwa baadhi ya mila na desturi zetu zinamkandamiza mwanamke. Baadhi ya mila hizo ni ile ya kumlazimisha mwanamke kuolewa na mtu asiyemtaka. Kama walivyofanya wazazi wa Yasmin kwa kumwozesha binti yao kwa nguvu kwa Bw. Raza. Yasmin hakumpenda Raza kwa sababu halikuwa chaguo lake. Hivyo, msanii anaonesha kuwa ili tujikomboe kiutamaduni lazima tuachane na mila hizo.

Pili, kuna mila ya kumweka mwanamke utawani, kama alivyofanya Shihab baada ya kumuoa Yasmin. Shihab baada ya kumuoa Yasmin alimweka utawani. Jambo hili linazorotesha maendeleo ya mwanamke, kwani badala ya kushughulika na kazi za kimaendeleo hukaa ndani tu na kusubiri kuletewa kila kitu na mwanaume. Katika kupiga vita mila hii msanii anaonesha kuwa, Yasmin alitoroka kwa shihab kwa lengo la kuonesha kuwa mila kama hizi zimepitwa na wakati na jamii haina budi kuzitupilia mbali mila hizo.

Hivyo, msanii anaishauri jamii kuwa, ili tuweze kujikomboa kiutamaduni hatuna budi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na
wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya jamii nzima kwa ujumla.

Ukombozi wa kisiasa​

Hapa msanii anazungumzia harakati za wananchi wa Unguja na Pemba za kujikomboa kutoka katika minyororo ya kunyonywa, kukandamizwa, kunyanyaswa na kuonewa na wakoloni wa Kiingereza pamoja na vijibwa vyao.

Katika kujadili hayo, msanii anaonesha wazi jinsi Denge na kundi lake wanavyojishughulisha na harakati hizo kwa kutawanya vitabu vyenye mawazo ya kijamaa, magazeti yanayopinga ukoloni na makaratasi mengine ya uchochezi dhidi ya wakoloni. Wao waliamini kuwa kwa kutumia vitabu, magazeti na makaratasi hayo, wananchi wa kawaida wangeamka na kuzijua haki zao na hatimaye kuanza kupambana na ukoloni huo.

Katika kujadili dhamira hii ya ukombozi wa kisiasa, msanii anaonesha kuwa lazima tuwe na watu waliojitolea muhanga katika harakati hizo. Denge na kundi lake walijitoa muhanga katika kuhakikisha kuwa nchi yao inakombolewa kutoka katika mikono ya wakoloni kama asemavyo Denge (uk. 145);

“Yasmin mimi najua unanipenda na mimi nakupenda vilevile, lakini kuna kitu kimoja napenda uelewe, kuna mapenzi na wajibu wa mtu katika jamii. Kila mtu ana wajibu fulani katika jamii na mimi wajibu wangu mkubwa ni kufanya kila niwezalo kwa kushirikiana na wenzangu ambao wengine unawajua na wengine huwajui ili kuona kwamba nchi hii inakuwa huru. Hii ni kazi ngumu ina matatizo mengi na inahitaji kujitoa muhanga na mimi ni miongoni mwa hao waliojitolea muhanga kufa, kupona, potelea mbali. Tupo wengi tuliojitolea namna hiyo, tena wengi sana, maelfu.”

Denge na kundi lake walifuatwa sana na askari, lakini hawakuacha kueneleza harakati zao za kudai uhuru.

Vilevile msanii anaonesha kuwa ili tujikomboe kisiasa, lazima tuwe na umoja na mshikamano, kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Denge na kundi lake walishirikiana sana katika harakati zao za kupambana na wakoloni.

SOMA UCHAMBUZI KAMILI HAPA>>>