Mfumo wa Anwani za Makazi NaPA Tanzania

wazaelimu

Administrator
Staff member
Jun 15, 2026
55
0
6
Fahamu kuhusu "Mfumo wa Anwani za Makazi NaPA Tanzania" NaPA inatumika kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu ya juu HESLB.

Faida za matumizi ya mfumo wa anwani za makazi na postikodi
  • Kurahisisha utoaji, upatikanaji na upelekeaji wa huduma na bidhaa kwa wanachi/wateja;
  • Inawezesha biashara mtandao na upatikanaji wa huduma nyingine za kijamii kama vile za afya;
  • Kutambua eneo kirahisi na kufahamu mahali alipo mtu au kitu hivyo kupunguza muda na gharama za usafiri;
  • Inaongeza kasi ya kupambana na uhalifu, kuimarisha shughuli za uhamiaji, utalii, ulinzi na usalama.
  • Kurahisisha upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali za maendeleo ya kibiashara na kijamii.
  • Inaongeza tija kwenye huduma za uokoaji na maafa;
Napa itakuwezesha;
1. Kujua anuani yako: Fahamu Anwani unayoishi na Anwani ya Taasisi
2. Tafuta Postikodi: Fahamu Postikodi ya eneo lako unaloishi
3. Tafuta Address Kodi: Fahamu Addresskodi ya eneo unaloishi
4. Barua ya Utambulisho: Pata Barua ya utambulisho wa ukaazi.